Mioyo Miongoni Mwetu

The Swahili translation of Hearts Among Ourselves by A. Happy Umwagarwa

About the Book

Karabo amepona mauaji ya kimbari dhidi ya Watusi mwaka 1994 ambayo yaliyatwaa maisha ya baba yake na wadogo zake. Sasa ameachwa peke yake miongoni mwa mioyo iliyojeruhiwa nchini Rwanda, na hafahamu mahali alipo mama yake.

Karabo alipokwenda kuishi na baba yake mkubwa, ambaye ni kanali kwenye jeshi jipya, anakutana na Shema, mhanga mwingine wa mauaji ya kimbari akiwa miongoni mwa walinzi vijana wa baba yake mkubwa. Tabasamu la Shema linamtetemesha, na Karabo anataka kuusalimisha moyo wake kwake, lakini mambo yanakuwa magumu — Shema anafahamu sehemu tu ya hadithi yake.

Mioyo Miongoni Mwetu ni simulizi ya mapenzi, chuki, na namna vinavyoingiliana. Karabo na Shema, wote wakiwa yatima wanaoomboleza, wanakulia kwenye jamii iliyochanwachanwa — ikitekwa katikati ya ulimwengu wa walio hai na wafu, na migogoro baina ya Wahutu na Watusi.

Leave a Message


    [anr_nocaptcha g-recaptcha-response]